Keifo FM

Kyela:Jinsi Samia alivyoshusha gari jipya Tafiri Kyela

5 October 2024, 10:20

Pichani kaimu mkurugenzi wa kituo cha Utafiti wa uvuvi Tafiri wilaya ya Kyela Dr Nestory  Gabagambi picha na James Mwakyembe

Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hasani ametoa gari jipya kwa kituo cha utafiti wa samaki wilaya ya kyela Tafiri ili kurahisisha utendaji kazi wa kituo hicho.

Na Nsangatii Mwakipesile

Kaimu mkurugenzi kituo cha utafiti wa uvuvi Tafiri Kyela Dr Nestory  Gabagambi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hasani kwa kuwapatia gari jipya kwajili ya kurahisisha uendeshaji wa shughuri mbalimbali wa taaasisi hiyo.

Akizungumza na keifo fm radio Dr Gabagambi amesema tangu kuanza kwa kituoa hicho cha utafiti hapa wilayani kyela hawajawahi kuwa na gari hali iliyokuwa inapelekea ugumu wa utekelezaji wa majukumu kwa wakati hivyo kupatikana kwa chombo hicho hivi sasa kutarahisisha utendaji kazi wa Tafiri.

Sauti ya kaimu mkurugenzi Dr Nestory P Gabagambi akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia gari jipya kituo cha kyela.

Dr Gabagambi ameleza majukumu makubwa ya TAFIRI kwa wilaya ya kyela ni kufanya tafiti za uvuvi kwenye kanda ya nyanda za juu kusini na kusini magaribi mikoa saba.

Sauti ya Dr Gabagambi akielezea kazi ya kituo cha kyela

Wakati huohuo  Dr  Gabagambi amewaomba watanzania hususani wanakyela kujitokeza  kwa wingi kwenye mkutano  wa mwaka wa utafiti unaotarajiwa kufanyika jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC.

Sauti ya Dr Gabagambi akiwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa mwaka utakao fanyika mkoani Arusha.
Miongoni mwa mashine zinazotumiwa na kituo cha utafiti wa samamki waliya ya kyela zikiwa zimehifadhiwa katika chumba maaluumu.

Taasisi ya utafiti wa uvuvi Tanzania alianzishwa mwaka 80 kwa sheria  ya bunge na 6 na ikaendelea kufanya kazi mpaka mwaka 2016 kabla ya kufanyiwa marekebisho na kuongezewa majukumu ambayo mpaka sasa inafanya kazi katika sheria hiyo.