Mwangasa: Nitaendelea kuabudu hapa nikiwa Kyela
1 July 2024, 18:03
Wakili msomi wa kujitegemea hapa nchini Tanzania Michael Mwangasa ameabudu katia kanisa la Jesus Desciples Tanzania na kuwapongeza waumini wa kanisa hilo kwa maombi waliyoyafanya wakati wote wa kesi ya Gerald Mwakitalu.
Na James Mwakyembe
Kwa mara ya kwanza tangu kufanikisha ushindi katika kesi iliyokuwa ikimkabiri mwanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Gerald Mwakitalu wakili msomi wa kujitegemea kupitia chama hicho Michael Mwangasa ameshiriki ibada katika kanisa la Jesus Desciples Tanzania lililopo katika kitongoji cha Ngorongoro kata ya Bondeni hapa wilayani kyela.
Hatua hii inakuja ikiwa ni takribani mwaka mmoja umepita tangu kuachiriwa huru kwa Gerald Mwakitalu baada ya kushinda rufaa yake katika kesi iliyokuwa ikimkabiri na kuhukumiwa kifungo cha maisha huku iliyotolewa na mahakama ya wilaya ya kyela.
Akizungumza katika ibada kanisani hapo baada ya kupewa nafasi ya kusalimia kanisa Mwangasa amewashukuru waumini wa kanisa hilo kwa maombi yao yaliyofanikisha kuachiriwa huru kwa mwakitalu huku akisema yote yaliyofanyika yalikuwa ni kuonesha upendo wa kweli kwa kanisa.
Katika hatua nyingine wakiri huyo msomi amesema pamoja na kushiriki ibada hiyo pia amegusia suala la utawara bora huku akisema chama hicho kitaendelea kusimamia msingi wake wa kusimamia demokrasia bora kwa wananchi wote hapa nchini ili taifa liweze kusonga mbele.
Awali akimkaribisha mbele ya waumini wa kanisa la Jesus Desciples Tanzania katibu mwenezi wa chama hicho Donald Mwaisango amewataka waumini kuendelea kukiombea chama chao ili kiweze kushika hatamu huku akisisitiza kuwa safari hii watahakikisha wanashinda chaguzi zote zilizombele ili uwogoza watanzania katika misingi bora ya kidemokrasia.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya kanisa mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Eliya Marko Mwakibwili yeye amemshukuru Mwangasa na kumtakia kila lakheri katika safari yake ya maisha ya kuwatetea wananchi kupitia taaluma yake ya uwakiri pamoja na kisiasa.
Huduma ya Jesus Desciples Tanzania ni huduma ya kiroho iliyopo kitongoji cha Ngorongoro kata ya Bondeni hapa wilayani kyela ikiwachini ya mbeba maono Askofu Gasper Ernest Chinyelese.