Waziri Mkuu ziarani Kyela
10 May 2024, 18:21
“Tupo tayari kumpokea waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ili aje aone namna fedha za zinazotolewa na raisi samia jinsi zinavyofanya kazi za maendeleo hapa wilayani”.
Na Masoud Maulid
Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa anatarajiwa kuzuru Kyela na kufanya ziara itakayoambatana na ukaguzi na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya kiserikali mwishoni mwa wiki hii.
Kwa muujibu wa mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase amesema waziri mkuu Kasimu Majaliwa anatarajiwa kuingia wilayani hapa jumapili na kufanya ukaguzi wa shamba la kokoa na shule ya wasichana mkoa wa mbeya inayojengwa katika kata ya Busale.
Ameongeza kuwa mbali na waziri mkuu kukagua miradi pia atatembelea shamba la kakao pamoja na kuweka jiwe la msingi katika jengo la wodi la mama na mtoto na pia kuweka jiwe la msingi kwenye shule ya wasichana mkoa wa Mbeya ambayo imejengwa kata ya busale hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi.
Kwa upande wa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya kyela wakizungumza kwa niaba ya wananchi wamesema,wamefurahishwa na ujio wa waziri mkuu Kassimu Majaliwa ndani ya wilaya ya kyela ambapo wameeleza kuwa ugeni huo unafungua fursa nyingi kwa wananchi,hivyo wamewataka wananchi kujitokeza katika mapokezi yake.
Ujio wa waziri mkuu Kasimu Majaliwa ndani ya wilaya ya Kyela unabeba matumaini kwa wananchi juu ya kutatuliwa kwa kero zao mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakabiri ikiwemo migogoro ya ardhi ambayo imekosa mwarobaini hapa wilayani Kyela.