Keifo FM

Kyela: Mwakalile aililia TARURA Bujonde

8 May 2024, 17:57

Pichani ni karavati linalounganisha kijiji cha Itope na Isanga katika kata ya Bujonde lililoathiriwa na mafuriko yaliyoikumba wilaya ya kyela picha na James Mwakyembe

Baada ya kuharibika kwa miundombinu ya barabara katika kata ya Bujonde hapa wilayani kyela diwani wa kata hiyo Aloyce Mwakalile ameiomba serikali kupitia wakala wa barabara mijini na vijijini kukarabati karavati la Isanga.

Na Nsangatii Mwakipesile

Kutokana na mafuriko yaliyo ikumba wilaya ya Kyela na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara na madaraja ya muda diwani wa kata ya Bujonde Aloyce Mwakalile ameiomba serikali kapitia wakala wa barabara Tarura kuboresha barabara na boksi karavati zilizohalibiwa na mafuriko hayo.

Haya yanajiri wakati mvua kubwa zikiendelea kunyesha ndani ya wilaya ya Kyela ambazo zimesababisha uharibifu wa mali za watu ikiwemo majengo na pahara kwingine kughalimu uhai wa watu.

Akizungumza na mwandishi wa Habari kutoka Keifo Fm Mwakalile   amesema pamoja na kadhia hiyo ya mafuriko lakini ameelekeza shukrani zake kwa  Rais wa jamhuri ya Mungano wa Tanzania Samia Siluhu Hasan kwa kupeleka miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika kata ya bujonde.

Sauti ya mwakalile kuhusu shukrani zake kwa raisi samia suluh hasani

Akizungumzia kuhusu uharibifu wa mindombinu ya barabara na boksi karavati Mwakalile amewaomba Tarura kufanya ukarabati katika karavati linalounganisha Kijiji cha Itope na Kijiji cha Isanga.

Sauti ya mwakalile kuhusu ombi la kujengewa karavati kijiji cha Isanga

Meneja Tarura Karim Mfungata ametoa pole kwa wananchi wilayani kyela huku akisema serikali imeendelea kuona uwezekano wa kuboresha miundombinu hiyo ili kuirejesha katika hali ya kawaida huku akiwaomba wananchi kuwa watulivu wakati huu ambapo serikali inaendelea kulishugulikia suala hilo.

Sauti ya Mfungata mhandisi wa tarura kuhusu pole yake kwa wananchi wa itope kyela
Pichani ni mhandisi wa TARURA wilaya ya Kyela Karim Mfungata

Kata ya Bujonde ni mwingoni mwa kata zinazokumbwa na mafuriko mara kwa mara  kutokana na kuwa mwishoni wa mto kiwira unao tiririsha maji yake kutoka wilaya ya Rungwe mkoani mbeya.