Najivunia Kyela yetu Festival 2024 sasa rasmi Kyela
7 May 2024, 18:24
Siku chache baada ya kuanza kutekeleza majukumu yake ya kusaidia jamii ya Kyela kikundi cha Najivunia Kyela Yetu kimezinduliwa rasmi ndani ya Kyela huku kikiweka mikakati yake kwa mwaka 2024.
Na Nsangatii Mwakipesile
Kikundi cha Najivunia Kyela Yetu Festival chenye maskani yake hapa wilayani Kyela mkoani Mbeya kinachojishughulisha na shughuli mbalimbali za kijamii kimezinduliwa rasmi huku milango ikifunguliwa kwa wadau mbalimbali wanaotaka kujiunga katika kikundi hicho.
Shughuli za uzinduzi zimefanyika katika ukumbi wa Sativa Midland Hotel hapa wilayani kyela huku mikakati madhubuti ya kikundi hicho ikiwekwa wazi pamoja na kuzitaja kazi zake kubwa zinazofanywa na kikundi hicho.
Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi Mwenyekiti wa Najivunia Kyela yetu Festival 2024 Aizack Mwaipape amesema Najivunia Kyela yetu ilianzia kwenye mtandao wa kijamii wa whatsap ukujumuisha wadau mbalimbali waliondani na nje ya kyela lengo likiwa ni kuisaidia jamii ya wanakyela ambapo katika kulifanikisha hilo tayari shughuli mbalimbali zimekwisha kufanywa mpaka kuzinduliwa kwake.
Mwaipape ameongeza kwa kuwataka wadau kutoka ndani na nje ya nchi kuendelea kujiunga na kikundi hicho kwalengo la kuimarisha umoja utakaokuwa na nguvu ya kutoa majibu kwa jamii ya wanakyela wanaokumbwa na kadhia mbalimbali.
Akitoa Tarifa ya utekelezaji ya kikundi cha Najivunia Kyela Yetu katibu wa kikundi hicho Abinyuti Mwakilewa amesema pamoja na malengo yaliyobainishwa na mwenyekiti wa kikundi lakini miongoni mwa malengo ya ilikuwa ni kuwasaidia wanakikundi kijikwamua kiuchumi na kisha kijamii.
Akishukuru kwa niaba ya wanakikundi hicho Vanesa Ngesyenge amesema anajisikia furaha kwasababu yeye ni muumini mkubwa wa kuisadia jamii na kuwapongeza viongozi kwa kujitoa na kufanikisha kusajiri na kuzindua kikundi hicho.
Umoja wa kikundi cha Najivunia Kyela yetu Festival 2024,umeanzishwa kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsap tarehe 28 Ogasti 2021 wakiwa na malengo ya kusaidiana katika shida na raha jambo ambalo sasa limevuka mpaka hadi kuifikia jamii ya wanakyela kwa misaada mbalimbali katika elimu na afya.