108 wakabidhiwa vyeti vya udereva Kyela
6 May 2024, 14:18
Katika kukabiliana na ajali za barabarani jeshi la polisi mkoa wa Mbeya limetoa vyeti kwa wahitimu miamoja na nane hapa wilayani kyela mbele ya mgeni rasmi afande RTO H.A Gawile.
Na Nsangatii Mwakipesile
Mrakibu wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani H.A Gawile amekabidhi vyeti vya kuhitimu kwa mafunzo ya udereva kwa madereva miamoja na nane hapa wilayani kyela ikiwa ni muendelezo wa jeshi hilo kushirikiana na wadau wengine kuwa na madereva welevu watakao saidia kupunguza wimbi la ajari hapa nchini.
Haya yamejiri katika ukumbi wa kanisa la Romani katoliki hapa wilayani kyela wakati wa shughuli za kuwatunuku vyeti wanafunzi waliohotimu mafuzno ya udereva katika chuo cha Mj driving school yakihudhuriwa na mgeni rasmi mrakibu wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani H.A Gawile.
Akikabidhi vyeti hivyo Mrakibu wa jeshi la polisi kitengo cha usala barabarani H.A.Gawile amewapongeza wakufunzi wa chuo cha Mj kwa namna walivyojitahidi kuwaandaa madereva hao huku akiwataka wamiliki wa vyuo vingine vya udereva kuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo kama hayo kwa waendesha pikipiki maarufu bodaboda.
H.A.Gawile ameongeza kwa kuwataka wahitimu hao kuhakikisha wanatii sheria bila shuruti pamoja kufuata sheria zote za usalama barabarani huku akisisitiza kuwa jeshi hilo litakuwa kali kwa madereva wote wanyekuvunja sheria za usalama wawapo barabarani
Kwa upande wa mkuu wa chuo cha MJ driving school kilichopo Uyole Mbeya Taslo Sanga yeye ametoa shukrani kwa kanisa katoliki hapa wilayani kyela pamoja na jeshi la polisi wilaya ya Kyela chini ya DTO Insecta Seif kwa ushirikiano walioutoa katika kufanikisha jambo hilo.
Wakizungumza kwa furaha baada ya kupokea vyeti vyao vya uhitimu wa mafunzo ya udereva hapa wilayani Kyela wamemshukuru afande H.A Gawile na chuo cha MJ driving School kilichofanikisha wao kupata vyeti vyao na kuiomba serikali kutilia mkazo chuo hicho kupata wanafunzi wengi zaidi ili kitambulike nchini kote.
Mafunzo ya udereva kwa madereva wa vyombo vya moto hapa wilayani Kyela yamehitimishwa kwa kukabidhi vyeti jumla ya madereva miamoja na nane ambao ni madereva wa vyombo mbalimbali vya moto ikiwamo magari ya abiria.