Keifo FM

Kyela:Madaktari na wauguzi wazembe sasa kukiona chamoto

30 April 2024, 14:10

Pichani Mwanyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Katule Kingamkono akiwa na viongpzi waandamizi wa hospitali ya wilaya ya Kyela wakati akihitimisha ziara yake.

Katika kuhakikisha kwamba huduma bora za afya zinapatikana katika zahanati,vituo vya afya na hospitali ya wilaya ya kyela serikali imekusudia kuwaondoa kazini watumishi wote walio na lugha mbaya ya matusi kwa wagonjwa hapa wilayani Kyela.

Na James Mwakyembe

Ziara ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela kutembelea zahanati zote ndani ya wilaya imehitimishwa rasmi katika hospitali ya wilaya Kyela huku onyo kali likitolewa kwa watumishi wazembe kuwa serikali haitawavumilia kuichafua wilaya.

Ziara hiyo imefanywa rasmi ikiwa na malengo mawili ambayo ni kutazama mapato ya zahanati ndani ya halmashauri pamoja na kutazama mambo mbalimbali ya kiutendaji baada ya kuwepo kwa taarifa kutoka katika baadhi ya zahanati kutokusanya fedha pamoja na kuzitumia nje na matumizi ya serikali.

Akizungumza wakati wa kukamilisha ziara hiyo akiwa katika hospitali ya wilaya ya Kyela Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Katule Godfrey Kingamkono amepongeza uongozi wa hospitali ya wilaya ya Kyela kukusanya mapato vizuri ambapo hospitali hiyo imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi milioni mia sita na nane kutoka katika makadilio ya bajeti yao ya shilingi milioni miasaba na hamsini.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya kyela Katule Kingamkono kuhusu pongezi na makusanyo kwa uongozi wa hospitali ya wilaya kyela

Pamoja na pongezi hizo alizozitoa kwa uongozi Katule ameongeza kuwa baraza la madiwa lilimwagiza mkurugenzi mtendaji kupitia idara ya afya kuhusu mifumo ya ukusanyaji mapato ambapo lilitolewa agizo la kuwaondoa mawakala waliopo sasa na kazi hiyo kufanywa na hospitali yenyewe.

Sauti ya mwenyekiti kuhusu kuwaondoa mawakala wanaokusanya mapato hospitalini hapo na kusimamia wao wenyewe.
Pichani ni madakatari na wauguzi wakiwa katika hitimisho la ziara ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela katika hospitali ya wilaya.

Katika hatua nyingine Katule amesema ili kuhakikisha mapato hayo yanakusanywa vizuri ni lazma kuboreshwe huduma za afya kwa ngazi ya zahanati,vituo vya afya hadi hospitalini ya wilaya ya Kyela ili kufanya watu wajivunie huduma zinazotolewa na serikali kisha kutoa kalipio kwa wauguzi wanaokiuka taaluma yao.

Sauti ya mwenyekiti halamashauri ya wilaya ya Kyela kuhusu uboreshwaji wa huduma pamoja na kalipio kali kwa wahudumu wazembe

Katika kuunga mkono uboreshwaji wa huduma za afya hospitalini hapo Kingamkono ametoa televisheni moja kubwa itakayofungwa eneo la kupumzikia watu walio na wagonjwa hospitalini hapo katika eneo lililojengwa upya baada ya lile la kwanza kuendolewa kupisha ujenzi wa barabara ya Ibanda- Itungi Port.

Sauti ya kingamkono kuhusu jengo kujengwa upya

Katule Godfrey Kingamkono ni diwani wa kata ya Ikimba hapa wilayani Kyela ambaye mwaka 2020 alichaguliwa na madiwani wenzake kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kyela ambapo mpaka sasa ameendelea kushikiria nafasi hiyo kwa kuwatumikia wananchi kuzitatua kadhia mbalimbali zinazowakumba katika maeneo yao.