Convenant Edible Oil Ltd yamwaga vifaa vya michezo Kajunjumele Kyela
27 March 2024, 13:01
Kampuni ya kuzarisha mafuta ya Kyela Cooking Oil Convenant Edible Oil Ltd chini mkurugenzi Babylon Mwakyambile wamekabidhi mipira nane kwa timu nane shiriki katika ligi ya chama cha Mapinduzi ccm kata ya Kajunjumele.
Na Nsangatii Mwakipesile
Mkurungenzi wa kampuni ya Convenant Edible Oil Ltd wazarishaji wa mafuta ya Kyela Cooking Oil Babylon Mwakyambile amakambizi Mipira Nane katika kata ya Kajunjumele yenye thamani ya zaidi ya shilingi laki nne hapa wilayani kyela.
Tukio hilo limefanyika mala baada ya kutamatika kwa mashindano ya chama cha mapinduzi [CCM] na kushawishi vijana kijisajiri katika mfumo wa kietroniki na kuchukua kadi ili kujenga afya kwa vijana ndani ya kata hiyo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hioyo hivyo kaimu Mwakirishi wa mkurugenzi Frenk Mwakapala amewasihi vijana kujituma na kucheza kwa malengo kwani kwa sasa mpira ni ajira.
Pia amewatoa hofu kwamba kamuni hiyo iko tayari kushiriikiana nao wakati wowote panapohitajika vifaa vya michezo ili kukuza vipaji vya vijana wa kata hiyo.
Kwa upande wa katibu wa Umoja wa vijana kata ya Kajunjumele Richard Mwaipungu amemshukuru Babylon Mwakyambile kwa vifaa hivyo huku akikiri kuwa kwa moyo aliouonesha ni moyo wa kizalendo na upendo kwa tarifa ya mwaliko aikuchukua muda mwingi hata kujibiwa maombi yao yaliyopelekea kupewa vifaa hivyo bora vya kimichezo vitakavyokuwa msaanda katika tasnia ya michezo kwao.
Pia wawakirishi wa timu zilizo shiliki kwenye mashindano hayo ya ndani ya kata ya Kajunjumele wameshukuru mdau huyo na kuahidi kwenda kutengeneza timu zao na kishiriki mashindano makubwa zaidi ndani na nje ya kata hiyo.
Timu zilizokabodhiwa mipira ni pamoja na,Mbeya City ya kajunjumele,Mbala Boy’s,Cossovo,Beach Boy’s,Soweto fc,Mapinduzi,New Boy’s,Mpanga fc.
Mashindano hayo yalianza tangu mwezi wa pili yakianza na timu kumi na nne ambapo timu nane zilizofanikiwa kusonga mbele kwa hatua ya robo fainali ndizo zimekabidhiwa mpira mmoja kwa kila timu.