Kyela:Mitungi ya Kinanasi yafika msikiti wa tenende
23 March 2024, 22:49
Mbunge wa jimbo la Kyela amendelea kukabidhi majiko ya gesi na sukari kwa waumini wa dini ya kiislamu ambapo mara hii amekabidhi majiko hayo katika misikiti ya tenende na Ipinda.
Na Masoud Maulid
Waislamu wilaya ya kyela wamempongeza mbunge wa jimbo la kyela Ally Mlaghila Kinanasi kwa kuwasaidia sukari kilo 40 na mtungi wa gesi kila msikiti, kwa lengo la kuchangia katika upatikanaji wa futari kwenye miskiti hiyo.
Hayo yamejiri baada ya katibu wa mbunge Edgar Mwasamlaghila kuendelea kukabidhi sadaka ya sukari na majiko ya gesi kwa niaba ya mbunge,ambapo waislam wa misikiti ya tenende na ipinda wamekuwa miongoni mwa mwaislamu ambayo wamekabidhiwa sadaka hiyo kwa lengo la kusapoti utaratibu wa kufuturu pamoja.
Akipokea sadaka hiyo kwa niaba ya waislamu wa msikiti wa tenende imamu Tabai amesema kitendo alichokifikilia mbunge kuwasaidia ameonyesha upendo kwa waislamu na uwe mfano kwa watu wengine waliojaliwa kuwa na kipato kuwasaida waislamu ndani ya ramadhani pamoja na watu wasiokuwa na uwezo.
Kwa upande wa katibu wa msikiti wa ipinda Omary Mohamedi amesema waislamu wa ipinda wameweka utaratibu wa kufuturu msikitini hapo kila mwezi wa ramadhani,hivyo sadaka aliyoitoa mbunge imekuja wakati sahihi huku akiongeza kuwa mbunge amekuwa akiwasaidia waislamu wa ipinda ikiwemo msaada wa vipazasauti.
Shekhe Abas Mwamloka ambaye ni kiongozi mkuu wa msikiti huo amesema,wananchi wa wilaya ya kyela wanatakiwa kuendelea kumuunga mkono kutokana na uchapakazi alionao pamoja na kuwa na moyo wa kujitoa kuwasaidia wananchi.
Mpaka sasa misikiti ambayo imepokea sadaka hiyo ya sukari kilo 40 pamoja na mtungi wa gesi ni pamoja msikiti mkuu wa wilaya,masjidi aqswa,masjidi,msikiti wa kalumbulu,msikiti wa tenende na msikiti wa ipinda ambapo zoezi linaendelea katika miskiti mingine iliyobaki