Nyani aingia ndani na kumjeruhi mtoto Kyela
8 March 2024, 16:09
Katika hali isiyokuwa ya kawaida nyani aina ya ngedere akiwa anakimbizwa kutoka sehemu nyingine kwenda sehemu nyingine gafla akikimbilia ndani na baadaye kumjeruhi mtoto.
Na Masud Maulid
nyani aliyekuwa anakimbizwa na watoto maeneo ya Majoka wialayni kyela ameingia ndani ya nyumba na kumjeruhi mtoto wa kiume anaesoma darasa la sita na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Nyani huyo baada ya kuona kundi la watu wengi aliamua kupanda juu nyumba na kujificha juu ya dali na kukaa huko kwa takriban saa mbili, kabla ya watu kupanda juu wakiwa na silaha mbalimbali likiwemo panga.
Baada ya muda mchache yale nyani akiwa anajiandaa kushuka ndipo akakutana na motto na kumjeruhi katika baadhi ya mwili wake na baada ya tukio hilo nyani aliweza kuuliwa na kundi la watu wakio kuwepo karibu na eneo hilo.
Jeshi la polisi limepewa taarifa, na kushauri kuwa taarifa wapewe wa tu wa maliasili ambao ndio wahusika wakuu wanao pambana na wanyama kwenye maeneo mbalimbali.
Baada ya taarifa kufikishwa kwa maafisa maliasili walisema ni vyema watu wakae mbali kidogo na eneo hilo ili nyani akiona utulivu atashuka mwenyewe baada ya kusikia ukimya.