Milioni mia nne kujenga kituo cha kupooza umeme kyela
7 March 2024, 15:51
picha,Mbunge Ally Mlagila akizungumza na wananchi
Serikali yaaja na mbinu mbadala ya kukomesha tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara wilayani kyela,
Na James Mwakyembe
Baada ya kuwepo katikakati ya umeme iliyokithiri serikali imetenga shilingi milioni mia nne kwa ajiri ya ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme wilayani Kyela.
Akizungumza na wananchi wilayani kyela Mbunge wa jimbo la Kyela Ali Mlagila amesema baada ya kuwepo kwa kadia ya kukatika kwa umeme imemlazimu kuiomba serikali kujenga kituo cha kupozea umeme wilaya hapa ili kunguza kadhia hiyo.
Sauti ya mbunge wa jimbo la kyela Ali Mlagila akizungumzia kuhusu kujengwa kituo.
Kuhusu lini ujenzi utaanza Mlagila amesema mpaka sasa tayari timu ya watalaamu kutoka serikalini imekwisha kuanza upembuzi yakinifu kujua eneo gani litafaa kwa ujenzi huo pamoja na kujua athari za kimazingira kambla hatua hazijachuliwa.
Sauti ya mbunge wa jimbo la kyela Ali Mlagila akizungumzia kuhusu upembuzi yakinifu
Kadharika mlagila amesema mkakati wa ujenzi na ukarabati wa mitambo ya kufua umeme kutoka kiwira Coal Mining tayari serikali imekwisha kukaa na timu ya watalaamu kutoka shirika la umeme Tanzania na tayari serikali imeridhia jambo hilo la kupata megawati hizo mia mbili.
Sauti ya mbunge wa jimbo la Kyela Ali Mlagila akizungumzia kuhusu mitambo ya umeme kiwira coal mining
Wilaya ya kyela ni miongoni mwa wilaya ambazo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto za kukatika kwa umeme hali inayosababishwa na kuwepo kwa kituo kimoja tu cha kupozea umeme Mwakibete kilichopo jijini Mbeya.