Recent posts
29 August 2023, 2:50 pm
Maofisa wa vyuo vya mafunzo Pemba watakiwa kubadilika
Na Is-haka Mohammed Pemba. Mtandao wa Utetezi wa Haki za Binadamu Tanzania umesema mwongozo wa malalamiko katika vizuizi (Vyuo vya Mafunzo) umewekwa kwa ajili ya kusaidia utatuzi wa changamoto na malalamiko ya walio vizuizini ili kutoa nafasi ya kushughulikiwa na taasisi…
29 August 2023, 2:32 pm
Wizara ya Afya Zanzibar yasambaza vifaa katika hospitali mpya za wilaya
Lengo la kujengwa hospitali za wilaya ni kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa kuwapunguzia masafa wananchi. Wizara ya Afya Zanzibar imesema kuanza kutumika hospitali za wilaya zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma kwa wananchi wa visiwa vya Unguja…
29 August 2023, 1:56 pm
Wazazi watakiwa kuwapeleka watoto hospitali kupatiwa huduma ya tohara
Wananchi wametakiwa kutumia fursa ya kwenda kufanya matibabu kwenye kambi inayoendelea katika Hospitali ya Kivunge. Na Omary Abdallah. Wizara ya Afya Zanzibar imesema kufanyika kwa kambi za magonjwa mbalimbali hapa nchini kunasadia kwa kiasi kikubwa kuwapatia huduma wananchi kwa ukaribu pamoja…
27 August 2023, 3:21 pm
Kijana ajinyonga Pemba
Na Is-haka Mohammed Mtu mmoja anayejulikana kwa jina Moh’d Omar Juma maarufu Magodoro anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 mkaazi wa Machomanne Kilimo amefariki dunia baada ya kuonekana akining’inia katika chumba kwa kujinyonga. Khamis Issa Moh`d ni Mwanafamilia wa…
25 August 2023, 3:56 pm
Tamwa Zanzibar yawanoa waandishi wa habari Pemba
Waandishi wa Habari Pemba wanatakiwa kufanya uchunguzi yakinifu kabla ya kurusha hewani habari za udhalilishaji. Na Is-haka Mohammed Pemba. Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa Zanzibar) kimewakumbusha waandishi wa habari juu ya umuhimu wa kuandika habari zenye tija na…
23 August 2023, 2:53 pm
Matukio ya udhalilishaji yaongezeka kwa 32.3% Zanzibar
Na Ahmed Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema pamoja na kupiga vita dhidi ya matukio ya udhalilishaji na ukatili kwa wanawake na watoto lakini bado matukio hayo yanaongezeka kila siku. Kwa mujibu wa takwimu za makosa ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia kutoka…
21 August 2023, 2:38 pm
CUF Pemba wailaumu ACT Wazalendo kushindwa kuwatetea wananchi
Chama cha Cuf Pemba imekitupia lawama chama cha Act Wazalendo kwa kushindwa kuisimamia Serikali ya Mapinduzi ya zanzibar katika swala zima la upandaji wa bei za bidhaa hasa vyakula. Na. Is-haka Mohammed Pemba. Chama cha Wananchi CUF kimetoa lawama kwa…
18 August 2023, 3:56 pm
Wafanyabiashara watakiwa kuhama pembezoni mwa barabara Zanzibar
Mkuu wa wilaya ya Magharibi B Hamida Mussa Khamis, amewataka wafanyabiashara wadogo wadogo wakiwemo wa matunda na mbogamboga kwenda kufanya biashara zao katika masoko ya muda yaliyopangwa na serikali ikiwemo Kwerekwe C, Kwerekwe Sheli pamoja na Soko la Jumbi. Na…
16 August 2023, 12:10 pm
Kipindi: Mwangaza wa habari
Na Ivan Mapunda. Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa kaskazini Unguja amewataka madereva kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali.
15 August 2023, 5:35 pm
Maafisa TRA, ZRA wafundwa Zanzibar
Na Ahmed Abdullah Maafisa kodi wa mamlaka ya mapato Zanzibar ZRA na mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wametakiwa kuwa na lugha nzuri kwa wateja ili kuwa na mahusiano mazuri baina ya mlipakodi na mamlaka hizo. Naibu kamishna wa Mamlaka ya…