Zenj FM

Hoogan: CHADEMA wamechelewa kudai tume huru ya uchaguzi

28 March 2025, 7:19 pm

Mwanasiasa na Mbunge wa zamani jimbo la Kikwajuni Parmukh Singh Hoogan.

Na Mwandishi wetu.

Mwanasiasa na Mbunge wa zamani jimbo la Kikwajuni Parmukh Singh Hoogan amesema wakati umefika na jamii ndogo ndogo kushilikishwa katika nafasi za uteuzi katika kuimalisha umoja wa Kitaifa.

Singh amesema hayo alipokuwa akizungumzia uchaguzi mkuu na nafasi za uongozi katika vyombo vya maamuzi.

Sauti ya Mwanasiasa na Mbunge wa zamani jimbo la Kikwajuni Parmukh Singh Hoogan.

Akizungumzia msimamo wa wapinzani kufungua kesi kudai Tume Huru ya Uchaguzi wakati imebakia miezi sita kufanyika uchaguzi mkuu Sawa na kupoteza muda.

Sauti ya Mwanasiasa na Mbunge wa zamani jimbo la Kikwajuni Parmukh Singh Hoogan.

Akigusia wanawake na uongozi amesema wameonyesha uwezo mkubwa na kutoa mfano wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania DK Samia Suluhu Hassan.

Sauti ya Mwanasiasa na Mbunge wa zamani jimbo la Kikwajuni Parmukh Singh Hoogan.

Hata huvyo amesema bado Kuna changamoto za uchumi na kuwapa wakati mgumu wananchi wanyonge.

Sauti ya Mwanasiasa na Mbunge wa zamani jimbo la Kikwajuni Parmukh Singh Hoogan.

Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu na tayari chama Tawala ( CCM) kimeteuwa wagombea wa urais Dk Samia Suluhu Hassan kuwania urais wa uungano DK Hussen Ali Mwinyi urais wa Zanzibar.