

20 March 2025, 3:25 pm
Na Kulwa
Baraza la Manispaa Mjini limewataka wafanya biashara wa vyakula kuzingatia sheria na kanuni za kufanya biashara hiyo kwa kukaa katika maeneo walio pangiwa nakuacha kufanya biashara hiyo katika maeneo ya pembezoni mwa barabara.
Afisa Afya na Mazingira wa Baraza la Manispaa Mjini Zelda Masoud ameyasema hayo wakati akizungumza na Zenji Fm, amesema serikali imechukua hatua za kuwaondoa mama lishe waliokuwa katika maeneo ambayo si rasmi na kuwahimiza wafanyabiashara wote kuhamia katika maeneo yanayotambulika rasmi na salama.
Aidha, Afisa Zelda Masoud amesema Baraza hilo litachukua hatua kali dhidi ya wale wote wanaoendeleza biashara ya vyakula katika maeneo yasiyo rasmi ili kuhakikisha usafi, usalama wa vyakula, na afya ya walaji.
Afisa Afya na Mazingira wa Baraza la Manispaa Mjini Zelda Masoud
Mwenyekiti wa wafanya biashara wa chakula katika maeneo ya Tigo yaliyopo Amani, wilaya ya Mjini, Hamad Mbaruk Khamis, ameiomba serikali kutoa eneo la kudumu litakalowezesha wafanyabiashara hao kufanya biashara katika mazingira salama.
Aidha Mwenyekiti amesema Ingawa wanakutana na changamoto, amewahimiza wafanyabiashara wa eneo hilo kuendelea kujitahidi na kuzingatia maelekezo ya serikali ili biashara zao ziwe salama na zizingatie sheria na kanuni zilizowekwa.
Mwenyekiti wa wafanya biashara wa chakula katika maeneo ya Tigo yaliyopo Amani, wilaya ya Mjini, Hamad Mbaruk Khamis.
Nae Ramadhan Mdau ,amewataka wafanya biashara hao kufunika vyakula vyao wakati huu wa vumbi ili kuweza kuzuia vumbi kwenye vyakula hivyo pamoja na kulinda afya za walaji.
Ramadhan Mdau
.