

6 February 2025, 4:37 pm
Na Mary Julius
Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar limesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inamipango mizuri kwa wananchi kwa kuweka mikakati madhubuti ya kuondoa tatizo la njaa nchini pamoja na umaskini.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM kisiwandui Makamo Mwenyekiti Baraza la Wazee wa CCM Zanzibar Waziri Mbwana Ali amesema serikali imeshapanga mipango ya kuhakikisha wananchi wote wanapata chakula cha kutosha kwa kuiendeleza sekta ya kilimo ili kupata chakula cha kutosha kwa wananchi pamoja na kuweza kuuza nje ya nchi.
Aidha Baraza hilo linawapongeza Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Hussein Ali Mwinyi kwa kuteuliwa na mkutano mkuu kugombea nafasi ya Urais kwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar
kuteuliwa kwao ni wazi wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar wanawaunga mkono kwa juhudi zao kutokana na uongozi wao.
Akizungumzia zoezi la uandikishaji wa wapiga kura wapya awamu ya pili Makamo Mwenyekiti amewataka vijana kujitokeza kujiandikisha ili kuweza kuwachagua viongozi wa ccm kwani ushindi a chama unategemea kura zao.