Awamu ya pili ya uandikishaji wapiga kura wapya Zanzibar kuanza Februari 2025
18 November 2024, 5:36 pm
Na Mary Julius.
Tume ya Uchanguzi Zanzibar (ZEC) imewaomba wananchi wenye sifa kushiriki katika wa awamu ya pili ya uandikishaji wa wapigakura wapya katika daftari la kudumu la wapiga kura, wakati utakapofika katika maeneo yao.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imewataka wananchi wenye sifa kujitokeza katika awamu ya pili ya uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kuanza tarehe moja mwezi wa pili mwaka 2025 (1/2/2025)
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ukumbi wa ofisi ya Tume hiyo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jaji George J. Kazi amesema kwa mujibu wa sensa ya watu na maakazi ya mwaka 2022 ,Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) inatarajiwa kuandikisha wapiga kura wapya sabini na nane elfu mia tisa ishirini na mbili (78, 922) waliotimiza umri wa miaka 18.
Mwenyekiti amesema uandikishaji wa wapiga kura wapya awamu ya pili unatarajiwa kuanza katika wilaya ya Micheweni na kumalizikia katika wilaya ya Mjini tarahe 17 march 2025 ambapo uandikishaji huo unatafanyika katika vituo 407 kwa muda wa siku tatu kwa kila shehia Unguja na Pemba.
Akizungumzaia mapitio ya mipaka ya majimbo ya uchaguzi mwenyekiti Jaji George amesema Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) haitachunguza idadi ya mipaka na majina ya majimbo badala yake yatabaki kama yalivyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Aidha mwenyekiti amesema Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imelazimika kufanya mabadiliko madogo ya mipaka ya majimbo ya wete na mtambwe kufuatia mabadiliko ya wadi yaliyofanywa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum kwa kuihamisha shehia ya limbani katika jimbo la Wete na shehia ya Mzambarau takao katika jimbo la Mtambwe.