Zenj FM

Zanzibar yaadhimisha siku ya takwimu Afrika

18 November 2024, 4:18 pm

Mtakwimu mkuu wa Serikali ya Mapinduzi  ya Zanzibar  Salum Kassim Ali, akizungumza na wandishi wa habari  katika kuadhimisha Siku ya Takwimu Afrika.

Na Belema Suleiman Nassor

Mtakwimu mkuu wa Serikali ya Mapinduzi  ya Zanzibar  Salum Kassim Ali amesema    takwimu zinazotelewa na ofisi ya mtakwimu mkuu  zinasaidia  Serikali  katika kupanga  mipango  ya maendeleo  ya sekta mbali mbali hapa nchini.

Ameyasema hayo katika  mkutano maalum  na wandishi wa habari  katika kuadhimisha Siku ya Takwimu Afrika amesema  vyombo vya habari  vina mchango mkubwa  kwenye jamii  katika kutoa  taarifa za kitaakwimu  kwa wananchi juu ya umuhimu wa matumizi sahihi ya takwimu katika kupanga maendeleo  kwa  jamii na taifa kwa ujumla.

Sauti ya Mtakwimu mkuu wa Serikali ya Mapinduzi  ya Zanzibar  Salum Kassim Ali

Nae Makamo Mwenyekiti wa Bodi  ya Takwimu  Zanzibar  Mary Khatibu amesema  lengo kuu la kuadhumisha siku ya takwimu Afrika ni kubadilishana mawazo pamoja na kuongeza ufahamu wa takwimu  rasmi uzalishaji usambazaji na ufikiaji na utumiaji wake  kwa ajili ya kufanya maamuzi na kupata ripoti kulingana na ushahidi sahihi wa kitakwimu.

Sauti ya Makamo Mwenyekiti wa Bodi  ya Takwimu  Zanzibar  Mary Khatibu.

Siku ya takwimu Afrika huadhimishwa kila ifikapo tarehe 18 Novemba  kwa Afrika.