Balozi Karume alia na ukuta unaozuia njia ya kuingia kwake
5 November 2024, 5:56 pm
Na Mwandishi wetu
Mtoto Rais wa kwanza wa Zanzibar Balozi Ali Karume amesema haikuwa muafaka barabara ya kuelekea nyumbani kwa marehemu mzee Karume kufugwa na kuanzishwa mradi wa ujenzi kiwanja cha michezo katika eneo la Maisara Zanzibar.
Balozi karume amesema hayo alipokiwa akizungumza na waandishi wa Habari katika nyumba ya Marehemu babayake hapo maisara mkoa wa mjini Magharibi Unguja.
Amesema nchi zote duniani zinalinda maeneo ya wazi ambayo yanatumiwa na jamii na majanga yanapotokea.
Balozi Karume amesema katika kuleta maendeleo serikali inapaswa kuzingatia suala la mipango miji kwa kuanzisha miji mipya katika maeneo megine ya nje ya mji katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Mradi wa ujenzi unaoendelea katika uwanja wa maisara umeibua mjadala mkubwa kwa wananchi. Wanasiasa na wanaharakati kutokana na eneo hilo kihistolia kutumika kwa shughuli za kijamii.