Zenj FM

Mafunzo kwa vikosi vya ulinzi kuimarisha utalii Zanzibar

22 October 2024, 5:37 pm

Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp. Hamad Khamis Hamad Akizungumza mara baada ya kukagua mafunzo yanayotolewa kwa kushirikiana baina ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na Jeshi la Polisi kwa Askari 43 wa Jeshi la Polisi na Askari wa Vikosi vya Idara Maalum ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Huko Chuo cha Polisi Zanzibar

Na Omar Hassan.

Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp. Hamad Khamis Hamad amesema mafunzo ya ulinzi wa mazingira,uokozi na usalama wa utalii wanayopatiwa Askari wa vikosi vya ulinzi na usalama yatasaidia kuimarisha ulinzi na hatimae kukuza sekta ya utalii na uchumi wa bluu nchini.

Akizungumza mara baada ya kukagua mafunzo yanayotolewa kwa kushirikiana baina ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na Jeshi la Polisi kwa Askari 43 wa Jeshi la Polisi na Askari wa Vikosi vya Idara Maalum ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Huko Chuo cha Polisi Zanzibar Cp. Hamad ameeleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa Askari watakuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa kiwango cha kimataifa.

Sauti ya Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp. Hamad Khamis Hamad.

Nae Mratibu wa Mafunzo hayo Dkt. Hassan Issa Ali kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema aweandaa masomo hayo kwa Askari ili kuwajengea uwezo na kuchangia kuwa na utalii unaojali mazingira salama.

Sauti ya Mratibu wa Mafunzo hayo Dkt. Hassan Issa Ali.

Kwa upande wao Sajenti Ramadhan Juma Shaaban na Koplo Neema Mabrouk ambao ni miongoni mwa Askari walioshiriki wamesema mafunzo hayo yamewaongezea uwezo na yatawasaidia kwenye utendaji wa kazi zao.

Sauti za Koplo Neema Mabrouk na Sajenti Ramadhan Juma Shaaban.

Mafunzo hayo yenye lengo la Kuimarisha Usalama wa Mazingira na Uchumi wa bluu yametolewa kwa muda wa wiki mbili.