Zenj FM

ZAECA yawafikia Madiwani Wilaya ya Kati

18 October 2024, 4:28 pm

 
Afisa Elimu kutoka Mamlaka ya Kuzuwia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) Yussuf Juma Akitoa elimu kwa Madiwani wa Baraza la Mji kuhusiana na kujiepusha na vitendo vya kupokea au kutoa Rushwa na Uhujumu Uchumi katika majukumu Yao.

Na Mary Julius.

Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu Mipango na Utawala, Ofisi ya Baraza la Mji Kati Rehema Khamis Hassan, amewataka Madiwani kufuata Sheria na kutoa Elimu dhidi ya Rushwa na Uhujumu uchumi katika Wadi zao.

Rehema ametoa wito huo katika mafunzo ya utoaji wa Elimu kuhusiana na Rushwa na Uhujumu uchumi kwa Madiwani na Watendaji wa Wilaya ya Kati Unguja, amesema lengo la mafunzo hayo  kwa madiwani hao ni kuwajulisha juu ya sheria na taratibu za kimsingi za uhujumu wa uchumi na rushwa.

Aidha Rehema amesema mafunzo hayo  yatawawezesha madiwani kujua nini cha kufanya wanapo ona ishara za uhujumu uchumi katika miradi ya maendeleo iliyopo katika wadi zao.

Sauti ya Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu Mipango na Utawala, Ofisi ya Baraza la Mji Kati Rehema Khamis Hassan,

Nae, Afisa Elimu kutoka Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu uchumi Zanzibar (ZAECA) Yussuf Juma, amewataka Madiwani kuhakikisha kua wanasimamia Sheria na taratibu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

         Aidha amesema ni jukumu la Madiwani kuhakikisha wanaunga mkono Juhudi za Serikali katika kupambana na Vitendo vya Rushwa na Uhujumu uchumi, pamoja na  kulinda Rasilimali za Nchi kwa kutoa taarifa katika Vyombo husika.

Sauti ya Afisa Elimu kutoka Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu uchumi Zanzibar (ZAECA) Yussuf Juma.

         Kwa upande wake Diwani wa Wadi ya Ubago  Ussi Ali Mtumwa, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti Baraza la Mji Kati, kwa niaba ya Madiwani wenzake  amesema wamefarajika kwa kupatiwa mafunzo hayo, ambayo yatawawezesha kubadilika katika utendaji wao wa kazi, pamoja na kuisaidi Serikali katika kuimarisha Miradi ya Maendeleo.

Sauti ya Diwani wa Wadi ya Ubago  Ussi Ali Mtumwa,