Zenj FM

Elimu ya mazingira kwa wafanyabiashara viwanda vya uchomeaji Wilaya ya Kati

2 October 2024, 3:35 pm

Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Ujenzi na Mazingira Baraza la Mji Kati Hadhar Abdalla Hadhar wa mwanzo kulia akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Miundombinu Ujenzi na Mazingira wakimpa elimu ya Mazingira, vifaa Kinga na Upimaji wa afya Mfanyabiashara wa Kuchomea katika eneo lake la kazi Tunguu kwa Shemego Wilaya ya Kati Unguja. 

Na Mary Julius.

Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Mazingira na Ujenzi Baraza la Mji Kati ambaye pia ni Diwani wa Wadi ya Tunguu Hadhar Abdalla Hadhar amewataka wafanyabiashara wa viwanda vya uchomeaji ( fundi wilding) wa Wilaya ya Kati Unguja kutunza mazingiara yanayo wazunguka.

Akizungumza katika ziara fupi ya kuwakagua wafanyabiashara hao iliyokuwa na lengo la kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wafanyabiashara wa  viwanda vya wachomeaji ili kufanya kazi zao katika hali ya utunzaji wa mazingira na kwa ufanisi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Mazingira na Ujenzi Baraza la Mji Kati Hadhar Abdalla Hadhar.

Kwa upande wake Afisa Afya na Mazingira Baraza la Mji Kati Salim Ali Tamimu amewataka wafanyabiashara hao kuwa na utamaduni wa kuvaa vifaa kinga kama vile miwani maalum, maski, glavu maalum, ovaroli pamoja na viatu vigumu kwaajili ya kujikinga na madhara yatokanayo na kazi zao.

Sauti ya Afisa Afya na Mazingira Baraza la Mji Kati Salim Ali Tamimu.

Nao  wafanya biashara hao wamesema wanakabiliwa na changamoto nyingi katika utendaji wao wa kazi ikiwa ni pamoja na gharama ya vifaa vya kutendea kazi, pia suala la kuhamishwa katika maeneo yao ya awali ya kutendea kazi jambo linalowapa wakati mgumu kwani gharama za ulipaji wa kodi zinawaathiri.

Sauti ya Wafanyabiashara.

Miongoni mwa maeneo yaliyo kaguliwa ni pamoja na Binguni, Tunguu, Jumbi na Kidimni.