Mafunzo ya Amali fursa kwa vijana kujiajiri
19 September 2024, 5:25 pm
Na Khalida Abdulrahman.
Vijana wameshauriwa kujiunga na vituo mbali mbali vya Mafunzo ya Amali ikiwemo mafunzo ya ufundi upishi na uchoraji ili kujiajiri wenyewe.
Akizunguimza na Zenji Fm Mwalimu wa skuli ya forodhani Sunskim Mwajuma Mussa Said akiwa katika maonyesho ya mafunzo ya amali katika viwanja vya Mnarani Kisonge Wilaya ya Mjini,amesema vijana na watuazima wanaopenda kujifunza elimu mbaadala wanatakiwa kutumia fursa kwa kujiunga na vituo hivo vya mafunzo ya amali ili kuwa na ujuzi tofauti ikiwemo kushona kudarizi pamoja na kupika.
Aidha mwalimu amewataka wazazi kuacha kuwachagulia fani za ujuzi watoto badala yake waawache watoto wasomee fani wanazo zitaka.
Nae Mwanafunzi Hidaya Ali Mohd anayesoma elimu mbadala amewashauri vijana waliokata tamaa wajiunga na elimu mbadala ili kufikia malengo na kujikwamua kiuchumi.