Hati za haki ya matumizi ya ardhi, kilimo mwarobaini migogoro ya ardhi Zanzibar
17 September 2024, 7:56 pm
Wanachi wametakiwa kufuata utaratibu ulio wekwa na kamisheni ya ardhi ili kupata vibali na kuondokana na migogoro ya ardhi.
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Rahma Kassm Aliy ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa utoaji wa hati za Haki ya matumizi ya ardhi na kilimo hafla ilo fanyika kikwajuni Zanzibar.
Aidha Waziri Rahma amewataka wanachi kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa na mamlaka husika ili kuweza kuepusha migogoro Mbali Mbali inayoweza kujitokeza baina Yao pamoja na kupatiwa nyaraka zinazotambuliwa na serikali.
Nae Katibu Mtendaji kutoka Kamisheni ya Ardhi Mussa Kombo Bakari amesema ni vyema jamii ikaendeleza na kukuza Mashamba ili yaweze kudumu Kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Akizungumza Kwa niaba ya wananchi wezake waliopatiwa hati miliki za ardhi za kilimo wanaishukuru serikali Kwa kuwapatia nyaraka hizo kwani kumepunguza changamoto Mbali mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili.