Zenj FM

Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba ahamasisha vita dhidi ya magendo Pemba

25 February 2026, 7:00 pm

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mgeni Khatib Yahaya akizungumza na taasisi mbali mbali za kuthiibiti magendo Pemba.

Na Is haka Mohammed.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mgeni Khatib Yahaya amezitaka taasisi za kuhiibiti magendo kisiwani Pemba kuendelea kushiriana na wananchi katika kuona biashara ya magendo inatokomezwa pamoja na kuzinimbau bandari bubu zilizopo katika maeneo ya kisiwa hicho ambazo ni sugu kwa kufanya magendo mbali mbali.

,Mkuu wa mkoa Mgeni amesyasema hayo wakati akizungumza na taasisi mbali mbali za kuthiibiti magendo Pemba  ikiwa ni kikao maalum kwa ajili ya ya kujadili namna bora ya kudhibiti biashara ya magendo kisiwani humo.

Amesema uingizwaji wa bidhaa za magendo pamoja na kuikosesha serikali mapato ya kodi pia husababisha kuingizwa kwa bidhaa dhaifu au zilizokosa sifa za kutumiwa na binadamu.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mgeni Khatib Yahaya.

Kwa upande wake Msaidiazi  Kamishana TRA Zanzibar Saleh Haji Pandu amesema suala la uingizaji wa magendo linapelekea athari kubwa kwa taifa na jamii hivyo kuwa na mikakati thabiti ya kuindoa ni kupunguza mzigo kwa serikali.

Sauti ya Msaidiazi  Kamishana TRA Zanzibar Saleh Haji Pandu.

Miongoni mwa taasisi ziilizoshiriki katika Warsha hiyo ya siku mbili ni pamoja na Kikosi cha Kuzuia Magendo Zanzibar KMKM, ZURA, ZAECA, ZRA