Zenj FM

Waziri Katambi aagiza polisi kupambana na uhalifu wa mtandao

11 February 2026, 8:59 pm

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Patrobas Katambi akizungumza na viongozi wa Jeshi la Polisi Zanzibar .

Na Denis Mtamwega.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Patrobas Katambi amelitaka Jeshi la Polisi kutumia kitengo cha Makosa ya kimtandao katika  kuthibiti matukio ya uhalifu dhidi ya mitandao ikiwemo utapeli wa mitandao na vitendo vya uvunjifu wa maadili vinavyoenda kinyume na tamaduni za nchi yetu.

Katambi ameyasema hayo wakati akizungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali wa Mikoa mitatu ya Unguja Zanzibar katika Ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Polisi Zanzibar.

Amesema, pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa katika kupambana na vitendo vya utapeli wa mtandao lakini bado wananchi wameendelea kutapeliwa, hivyo ameliagiza Jeshi la Polisi kuona umuhimu wa kuongeza jitihada katika kudhibiti matukio hayo.

Aidha amelitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya madereva wanaoendesha vyombo vya moto kinyume na sheria jambo ambalo linamekuwa kero kwa wananchi.

Sauti ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Patrobas Katambi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud (Mb) Amesema Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Jeshi la Polisi kuwa ndio msingi mkuu wa usalama na amani ndani ya nchi, hivyo serikali itaendelea kuboresha mazingira mazuri ya kazi na stahiki kwa Jeshi la hilo.