Zenj FM
Zenj FM
5 January 2026, 9:22 pm

Na Omar Hassan.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene, amewataka maafisa wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya haki, usawa, weledi na uadilifu wanapotekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi.
Akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Askari uliofanyika katika Chuo cha Polisi Zanzibar Waziri Simbachawene ametoa maelekezo kwa maafisa wakaguzi na askari kutoka mikoa mitatu ya Unguja, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuheshimu utawala wa sheria na kuwa na uwajibikaji wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Kwa upande wake, Kamishna wa Polisi Zanzibar, CP Kombo Khamis Kombo, amewasihi maafisa, wakaguzi na askari waliohudhuria baraza hilo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.
Naye Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, DCP Zuber Chembela, akiwasilisha salamu za shukrani, ampongeza Waziri Simbachawene kwa kutenga muda wake pamoja na majukumu mazito ya Wizara na kwamba ameahidi kutekeleza yale yote aliyoagiza ili kupata matokeo chanya.