Zenj FM
Zenj FM
26 November 2025, 5:39 pm

Na Omar Hassan.
Taasisi zinazohusika kuzuia na kupambana na usafirishaji haramu wa binaadamu zimetakiwa kutumia ubunifu wa kubaini vyanzo vya uhalifu huo ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikiwaathiri zaidi wanawake na watoto.
Akifungua Kikao cha Wadau wa Serikali kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano katika kuzuia na kupambana na uhalifu wa usafirishaji haramu wa binadamu Zanzibar, Mwembe Madema Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Siajabu Suleiman Pandu, ameisihi jamii kutoa taarifa za matukio ya usafirishaji haramu kwa mamlaka zinazohusika ili ziweze kuchukuliwa hatua.
Afisa Mwandamizi wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji haramu wa binaadamu Rafii Said Mnete amesema Serikali kupitia Sekretarieti hiyo imejipanga kuchukua hatua mbalimbali kuzuia na kukabiliana na matukio ya usafirishaji haramu wa binadamu nchini.
Nae Naibu Katibu wa Sekretarieti hiyo Kanda ya Zanzibar Huzaimat Bakar Kheir amesema lengo la kuzikutanisha Taasisi hizo ni kukuza ushirikiano katika kuzuia na kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu.