Zenj FM

Makosa ya kimtandao yatahadharishwa Zanzibar

13 November 2025, 3:48 pm

Jamii imeaswa kuacha tabia ya kutumia mitandao ya kijamii kuwaumiza na kuwadhalilisha watu wengine, kufanya hivyo ni uvunja haki za watu na kinyume na sheria za nchi.

Na Omar Hassan

Jamii imeaswa kuacha tabia ya kutumia mitandao ya kijamii kuwaumiza na kuwadhalilisha watu wengine, kufanya hivyo ni uvunja haki za watu na kinyume na sheria za nchi.

Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo Watendaji wa Madawati ya Jinsia na watoto, katika Chuo cha Polisi Zanzibar Wakili na Mwanasheria wa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Polisi Zanzibar, Mkaguzi wa Polisi (INSP) Sadiki Ali Sultan amesema kumtisha, kumsumbua, kumshurutisha au kumuumiza kihisia mtu kwa kutumia mitandao ni kinyume na kifungu cha 23 (1) cha Sheria ya makosa ya Kimtandao, ambapo adhabu yake ni faini isiyopungua milioni tano au kifungo kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

Sauti ya Wakili na Mwanasheria wa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Polisi Zanzibar, Mkaguzi wa Polisi (INSP) Sadiki Ali Sultan.

Mtendaji wa Dawati la jinsia na watoto kutoka Makao Makuu ya Polisi Stafu Sajenti Makame Khatibu Makame na Afisa hifadhi kitengo cha Mtoto kutoka Idara ya Ustawi wa Jamii Fatma Maulid ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo ya namna kushughulikia makosa ya udhalilishaji wa kijinsia na watoto wamesema mafunzo hayo yamewajenga kushughulikia kesi za udhalilishaji kwa ufanisi.

Sauti za Stafu Sajenti Makame Khatibu Makame na Afisa hifadhi kitengo cha Mtoto kutoka Idara ya Ustawi wa Jamii Fatma Maulid.