Zenj FM

UNICEF yasifu juhudi za Jeshi la Polisi kukomesha udhalilishaji wa kijinsia

12 November 2025, 3:57 pm

Baadhi ya watendaji wa Madawati ya Jinsia na watoto ya Jeshi la Polisi wa Mikoa ya Unguja wakishiriki katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa Mikoa ya Unguja huko Chuo cha Polisi Zanzibar.

Na Omar Hassan.

Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Katiba na Sheria Afisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mzee Ali Haji ameshauri kuangaliwa kwa kina sababu zinazopelekea kuongezea kwa vitendo vya udalilishaji wa kijinsia ili hatua za kupunguza udhalilishaji zichukuliwe.

Akifungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa Madawati ya Jinsia na watoto ya Jeshi la Polisi wa Mikoa ya Unguja huko Chuo cha Polisi Zanzibar amesema Serikali inafanya Jukudi kubwa katika kuzuwia, kubaini na kukabiliana na makosa hayo lakini bado yamekua yakiongezeka.

Sauti ya Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Katiba na Sheria Afisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mzee Ali Haji.

Nae Afisa Hifadhi ya Mtoto kutoka Shirika la UNICEF Ahmed Rashid Ali amesifu utendaji wa Madawati ya Jinsia na Watoto ya Jeshi la Polisi na kueleza kuwa uanzishwaji wa Ofisi za Dawati katika kila kituo cha Polisi ni miongoni mwa mafanikio katika kushughulikia kesi za udhalilishaji.

Sauti ya afisa Hifadhi ya Mtoto kutoka Shirika la UNICEF Ahmed Rashid Ali.

Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsia na Ulinzi wa mtoto Zanzibar, Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Ali Mohamed Othman amesema kumekuwa na mwitiko mdogo wa wananchi kuhudhuria katika vikao vya kufikisha elimu ya kupinga udhalilishaji kwa jamii pindi Watendaji wa Madawati wanapokwenda kutoa elimu kwa jamii.

Sauti ya Mkuu wa Dawati la Jinsia na Ulinzi wa mtoto Zanzibar, Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Ali Mohamed Othman