Zenj FM
Zenj FM
6 October 2025, 8:06 pm

Kutoka. ZEC.
Tume ya Uchaguzi imeanza ziara ya kutembelea Afisi za Uchaguzi za Wilaya ikiwa ni hatua ya kuhakikisha maandalizi ya Uchaguzi Mkuu 2025 yanafanyika kwa uwazi na ufanisi.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Jaji George J. Kazi amesema lengo kuu la ziara hiyo ni kuangalia utayari wa kuendesha Uchaguzi Mkuu 2025, pia kuhakikisha vifaa vinavyohitajika katika vituo vya kupigia kura vinapatikana kwa wakati.
Wakati wa ukaguzi huo, Mwenyekiti amesema katika , Afisi zote za Wilaya wamejiridhisha kwa asilimia 95 % vifaa vyote vipo na vimepangwa vizuri na Tume ipo tayari kwa ajili ya Uchaguzi na Tume haitarajii kuchelewa kufunguliwa vituo vya Kupigia Kura kutokana na changamoto ya vifaa vya Kupigia Kura.
Nao Maafisa Uchaguzi wa Wilaya wamesema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na hakuna changamoto yeyote iliyojitokeza kwa upande wao.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeanza ziara hiyo kwa kutembelea Afisi tatu za Tume ya Uchaguzi za Wilaya ambazo ni Afisi ya Tume Wilaya ya Magharibi ‘A’,’B’ na Wilaya ya Kusini.