Zenj FM

TRA yapanua wigo wa biashara ya maji Zanzibar hadi Tanzania Bara

16 September 2025, 4:27 pm

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Juma Mwenda akizungumza na uongozi wa kiwanda cha maji cha DROP OF ZANZIBAR huko Jendele Mkoa wa kusini Unguja.

Na Mary Julius.

Mamlaka ya Kodi ya Mapato Tanzania (TRA) imesema mfumo mzuri wa Kodi kwa bidhaa umeanza kuandaliwa ili maji yanayozalishwa Zanzibar yaweze kutumia soko la pamoja la Tanzania.
Hayo yameleezwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Juma Mwenda alipokuwa akizungumza na uongozi wa kiwanda cha maji cha DROP OF ZANZIBAR huko Jendele Mkoa wa kusini Unguja.

Sauti ya Kamishina mkuu wa mamlaka hiyo Yusuf Mwenda.

Aidha amesema TRA itaendelea kuimarisha huduma za forodha ili bidhaa ziweze kutoka kwa wakati kwa kushirikiana na mamlka nyingine za serikali.

Sauti ya Kamishina mkuu wa mamlaka hiyo Yusuf Mwenda.

Hata huvyo amewapongeza Kampuni hiyo kwa kuanza kutumia soko la Maji la nchini Comoro hatua ambayo itasadia kuitangaza Zanzibar kibiashra.

Sauti ya Kamishina mkuu wa mamlaka hiyo Yusuf Mwenda.

Kamishina Mwenda amesema wakati umefika wazalishaji wa maji Zanzibar kutumia Kodi Stempu ya kielektroniki katika kulinda viwango vya ubora wa bidhaa zao.

Sauti ya Kamishina mkuu wa mamlaka hiyo Yusuf Mwenda.

Upande wake Meneja Utawala katika kiwanda hicho Mahmond Hassan Bakary amesema wanakabiliwa na chagamo kubwa ya mizigo kutokutoka kwa wakati katika bandari ya Malindi na Maruhubi pamoja na huduma za umeme.

Sauti ya Meneja Utawala katika kiwanda hicho Mahmond Hassan Bakary.

Ziara ya Viongozi wakuu waandamizi katika Mamlaka ya Kodi ya Mapato Tanzania imeleta faraja kwa wazalishaji wa Maji Zanzibar ambao wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kushindwa kutumia soko la Maji la Tanzania bar kitokana na vikwazo.