Zenj FM

ACT Wazalendo yapongeza polisi, yatoa wito wa uhuru wa kazi

5 September 2025, 6:51 pm

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman akiwa pamoja na Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Kombo Khamis Kombo huko makao Makuu ya Polisi kamisheni ya Zanzibar.

Na Omar Hassan.

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo ambae pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman amewapongeza watendaji wa Jeshi la Polisi kwa utendaji mzuri na amehimiza Jeshi hilo lifanye kazi kwa uhuru na lisitumike na wanasiasa kwa maslahi yao binafsi.
Othman ametoa pongezi hizo akiwa na viongozi wa chama hicho wakati walipo kutana na Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Kombo Khamis Kombo Makao Makuu ya Polisi kamisheni ya Zanzibar na kuahidi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kudumisha Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Othman Masoud Othman.

Nae Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Kombo Khamis Kombo amempongeza Masoud pamoja na Ujumbe wake kwa ziara yao Makao Makuu ya Polisi, ambapo amewaomba viongozi wa Vyama vya Siasa kuendelea kuhubiri amani kwa wanachama wao ili hali ya Amani, utulivu na usalama iendelee kuwepo, wakati na baada ya uchaguzi Mkuu 2025.

Sauti ya Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Kombo Khamis Kombo.