Zenj FM
Zenj FM
4 September 2025, 5:09 pm

Na Mary Julius.
Mkuu wa Mkurugenzi wa Elimu ya Wapiga Kura na Mawasiliano kwa Umma wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, Juma S. Sheha, amesema tume hiyo imejipanga kikamilifu kuhakikisha watu wenye mahitaji maalum wanashiriki ipasavyo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Akizungumza na Zenji FM, Juma amesema ZEC imeandaa vitambulisho maalum kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum, wakiwemo watu wenye ulemavu, ili kuwapa kipaumbele wanapofika katika vituo vya kupigia kura.
Amesema Tume hiyo pia imeandaa kifaa maalum cha nukta nundu kwa ajili ya watu wenye changamoto ya uoni, ili kuwawezesha kupiga kura wao wenyewe bila kuhitaji msaada kutoka kwa mtu mwingine.
Aidha,ameiomba jamii kutowaficha watu wenye ulemavu bali wawahimize kushiriki kikamilifu katika zoezi la uchaguzi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Jumuiya za Watu Wenye Ulemavu Zanzibar SHIJUWAZA, Ali Machano ametoa wito kwa watu wenye ulemavu kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi kwani haki ya kupiga kura ni haki ya kila raia wa Zanzibar.
Mkurugenzi Ali amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga kuhakikisha ulinzi na usalama vinadumishwa wakati wa uchaguzi mkuu.
Aidha Amesema Tume ya Uchaguzi ZEC pia imeweka mkakati wa kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika mazingira shirikishi na rafiki kwa watu wenye ulemavu,
Shirikisho la Jumuiya za Watu Wenye Ulemavu Zanzibar SHIJUWAZA limeandaaa majukwaa kwa ajili ya kuwahamasihsha watu wenye ulemavu kushiriki katika shughuli za kisiasa na uchaguz mkuu wa october 2025.