Zenj FM
Zenj FM
29 August 2025, 5:50 pm

Kamishna wa Polisi Zanzibar, CP Kombo Khamis Kombo.Na Mary Julius.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, CP Kombo Khamis Kombo, ameweka wazi mikakati ya Jeshi la Polisi kuhakikisha usalama na amani wakati wa kampeni na uchaguzi.
Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari huko makao makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar, CP Kombo amesema jeshi limejizatiti kuhakikisha wananchi wanashiriki katika kampeni kwa usalama, huku wakifanya doria katika maeneo ya mjini na vijijini ili kudhibiti matukio ya kihalifu, kama vile wizi, ambavyo mara nyingi hutokea kipindi cha kampeni.
Aidha, CP Kombo amesema Jeshi la Polisi limejipanga kukabiliana na uhalifu wa mitandaoni, akisisitiza kudhibiti habari za upotoshaji ambazo zinaweza kuleta machafuko.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, CP Kombo Khamis Kombo.Kamishna Kombo amewaasa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani, akisema ni muhimu kutojaza magari kupita kiasi ili kuepuka ajali na vifo.
Kwa upande mwingine, CP Kombo amewakumbusha waandishi wa habari umuhimu wa kutoa taarifa sahihi, kwani lengo kuu ni kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani, na utulivu.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, CP Kombo Khamis Kombo.