Zenj FM
Zenj FM
28 August 2025, 5:38 pm

Na Mary Julius.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, Thabit Idarous Faina, ametangaza kuwa zoezi la uchukuaji wa fomu za uteuzi kwa ajili ya nafasi ya urais, uwakilishi, na udiwani limeanza rasmi leo.
Mkurugenzi Faina amesema kuwa zoezi hilo litaanza kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchukua fomu ya nafasi ya urais mnamo Agosti 30, 2025, saa 4:00 asubuhi, katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ZEC.
Kwa wagombea wa nafasi za uwakilishi na udiwani, Mkurugenzi amesema watachukua fomu katika ofisi za wilaya, ambako maofisa wa jimbo wako tayari kutoa huduma.
Aidha, Mkurugenzi amesema katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Tume yanatarajia kutumia Shilingi bilioni 12 kwa ajili ya shughuli zote za uchaguzi.