Zenj FM

Waandishi wa habari wasisitizwa kuzingatia maadili kuelekea uchaguzi mkuu 2025

27 August 2025, 6:55 pm

Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Suleimani Khamis,akiwa na Meneja Kitengo cha za Utangazaji TCRA Andrew Kisaka wakati akifungua mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kuripoti habari za uchaguzi.

Na Mary Julius.

Waandishi wa habari wametakiwa kuzingatia maadili ya taaluma yao katika kuripoti taarifa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ili kulinda amani, mshikamano na utulivu wa kitaifa.
Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Suleimani Khamis, ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kuripoti habari za uchaguzi amfunzo yaliyo fanyika katika ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar.
Amesema mafunzo hayo yamelenga kuwapatia waandishi mbinu sahihi za uandishi wa habari, ili kuhakikisha jamii inapata taarifa za kweli zisizoegemea upande wowote.

Sauti ya Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Suleimani Khamis.

Kwa upande wake , Mwanasheria wa Tume ya Utangazaji, Khadija Mabrouk Hassan, amesema kanuni za huduma za utangazaji wakati wa uchaguzi zinalenga kuhakikisha habari zote zinazoripotiwa zinakuwa za kweli, sahihi na zenye kuzingatia usawa.

Sauti ya Mwanasheria wa Tume ya Utangazaji, Khadija Mabrouk Hassan.

Akitoa mada katika mafunzo hayo Meneja Kitengo cha za Utangazaji TCRA Andrew Kisaka amewataka waandishi wa habari kuzitumia kalamu zao vizuri ili kuiepusha nchi kuingia katika machafuko.

Sauti ya Meneja Kitengo cha za Utangazaji TCRA Andrew Kisaka.

Nao baadhi ya waandishi wa habari waliopatiwa mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yamekuja kwa muda muafaka na watayatumia katika kuhakikisha kalamu zao zinajenga taifa.

Sauti ya waandishi.

Mada tatu zaliwasilishwa katika mafunzo hayo kanuni za huduma za utangazaji wakati wa uchaguzi, mwongozo wa utangazaji kuhusu machafuko na majanga yanayotokea kipindi cha uchaguzi na ya mwisho ni udhibiti wa ubora wa vipindi vya utangazaji.