Zenj FM

Ni rasmi! uchaguzi mkuu Zanzibar kufanyika oktoba 29, kura ya mapema oktoba 28

18 August 2025, 3:21 pm

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ZEC, Jaji Joseph J. Kazi, akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Jaji Joseph Kazi, uliopo katika ofisi za Tume hiyo Maisara Zanzibar.

Na Mary Julius.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ZEC, Jaji Joseph J. Kazi, ametangaza rasmi kuwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kwa mwaka 2025 utafanyika siku ya Jumatano, tarehe 29 Oktoba 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Jaji Joseph Kazi, uliopo katika ofisi za Tume hiyo Maisara, Jaji kazi amesema kwa mujibu wa Kifungu cha 34(3) na (4) cha Sheria ya Uchaguzi Na. 4 ya mwaka 2018, Tume imekamilisha na kupanga ratiba kamili ya shughuli zote muhimu kuelekea uchaguzi huo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ZEC, Jaji Joseph J. Kazi.

Kuhusu kura ya mapema , Jaji Kazi ametangaza kuwa upigaji kura ya mapema utafanyika Jumanne, tarehe 28 Oktoba 2025, siku moja kabla ya uchaguzi mkuu.
Mwenyekiti Jaji kazi amesema kura ya mapema itahusisha watendaji wanaosimamia majukumu ya Uchaguzi siku ya Uchaguzi, wakiwemo Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasaidizi Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi wa Vituo, Askari Polisi watakaokuwa kazini siku ya Uchaguzi, Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi, Watendaji wa Tume na Wapiga Kura ambao watahusika na kazi ya ulinzi na usalama siku ya Uchaguzi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ZEC, Jaji Joseph J. Kazi.

Aidha, Mwenyekiti amevikumbusha vyama vya siasa na wagombea kufuata Sheria, Kanuni na Miongozo ya Tume ya ili uchaguzi uendeshwe kwa uwazi, haki, na amani.

Sauti ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ZEC, Jaji Joseph J. Kazi.