Zenj FM

CP Kombo, elimu imezaa matunda dhidi ya udhalilishaji Zanzibar

7 August 2025, 4:00 pm

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Kombo Khamis Kombo.

Na Omar Hassan.

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Kombo Khamis Kombo, amewapongeza watendaji wa madawati ya Jinsia na watoto ya Jeshi la Polisi Tanzania kwa utendaji wao mzuri na kupelekea kupungua kwa makosa ya udhalilishaji.

Akiwakaribisha watendaji 245 wa Madawati ya Jinsia na watoto kutoka Mikoa yote ya Tanzania waliofika Zanzibar kwa lengo la kutoa elimu ya kupinga vitendo vya udhalilishaji kwa jamii, huko Chuo cha Polisi Zanzibar Kamishna Kombo amesema, juhudi za Jeshi la Polisi za kutoa elimu ya kupinga vitendo vya udhalilishaji zitapelekea kupunguza kwa vitendo hivyo.

Sauti ya Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Kombo Khamis Kombo.

Nae Mkuu wa Mtandao wa Polisi wanawake Tanzania Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Pili Mande, amesema elimu hiyo ya siku tatu itakayotolewa kwa Mikoa mitatu ya Unguja ni kuifanyia kazi kampeni ya Jeshi la Polisi ya “Tuwaambie kabla ya hawajaharibiwa”

Sauti ya Mkuu wa Mtandao wa Polisi wanawake Tanzania Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Pili Mande.

Nae Mkuu wa Polisi Jamii Zanzibar, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Jonas Mahanga, amesema Kitengo cha Polisi Jamii Zanzibar, kitaendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuzuia vitendo vya udhalilishaji pamoja na makosa mengine.

Sauti ya Mkuu wa Polisi Jamii Zanzibar, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Jonas Mahanga.