Zenj FM
Zenj FM
18 June 2025, 1:44 pm

Na Mary Julius.
Mamlaka ya Kodi ya mapato Tanzania (TRA) Zanzibar imesema imefanikiwa kuvuka malengo ya kukusanya kodi kwa asilimia 106 tangu kushauriwa kufungua matawi ya huduma katika ukanda wa utalii na Viongozi wakuu Rais wa Muungano Dk Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dk Hussen Ali Mwinyi.
Hayo yameleezwa na Naibu Kamisha wa Mamlaka ya Kodi ya mapato Tanzania (TRA) Zanzibar Saleh Haji Pandu alipokuwa akizungumzia utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2024/ 2025.
Aidha amesema mapato ya kodi yote yanayokusanywa hubakia Zanzibar na kutumika kwa shughuli za maendeleo na huduma za jamii.
Pandu amesema huduma za mtandao TRA zimeimalika na wafanya biashara wanaweza kukamilisha taratibu za malipo kabla mzigo kufika Zanzibar.
Amesema katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 TRA imejipanga kusimamia maadili na kupambana na mianya ya ukwepaji Kodi.
Akiwasilisha makadirio na matumizi ya bajeti ya mwaka wa Fedha na Mipango Zanzibar Saada Mkuya Salum amesema serikali imepanga kutumia shilingi tirioni 6. 9 mwaka 2025/ 2026.
Saada Mkuya Salu.Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaendelea kujadili bajeti kuu ya serikali kabla ya Baraza kuvunjwa na kufanyika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.