Zenj FM

Wanawake Pemba waombwa kujitokeza na kuepuka makosa ya uchaguzi uliopita

16 June 2025, 6:16 pm

Salma Omary Venny kutoka ZAFELA akizungumza na wanawake kutoka katika Jumuiya za wanawake, kutoka katika vya vya siasa na taasisi za dini Pemba juu ya uungaju mkono wanawake katika Uchaguzi mkuu na kuweza na kuweza kushinda.

Na Is-haka Mohammed

Wakati vyama mbali mbali vya siasa vikiwa vinaendelea na michakato mbali mbali ikiwemo ya kupata wagombea watakao viwakilisha vyama hivyo katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu 2025, wanawake Kisiwani Pemba wameombwa kutorejea makosa yao ya kila mwaka wa uchaguzi na wasimame pamoja kwa kuwaunga mkono wagombea wanawake watakaogombea.
kushikamana na kukuza ushiriki katika uongozi wa vyama vya siasa kwa lengo la kupata haki sawa katika nafasi uongozi ili kutowa maamuzi yatakayosaidia katika mambo yanayowakabili.
Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Jumuiya ya Mazingira na Utetezi wa Kijinsia Pemba (PEGAO) Hafidh Abdi Said wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa Asasi za Wanawake Pemba uliofanyika katika ukumbi wa Tamwa Pemba huko Mkanjuni Chake Chake Pemba.
Said amesema kwa mujibu wa takwimu za tume ya uchaguzi wanawake walioandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga Zanzibar ni asilimia 56% hivyo kuna nafasi kubwa zaidi kwa wanawake kuweza kushinda kwenye chaguzi hizo kama wataunganisha nguvu zao.

Sauti ya Mkurugenzi wa Jumuiya ya Mazingira na Utetezi wa Kijinsia Pemba (PEGAO) Hafidh Abdi Said.

Aidha Said Abdala kutoka Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar Juwauza na Salma Omar Zenny wameeleza umuhimu wa wanawake kupata nafasi ya uwakilishi katika nafasi za uongozi.

Sauti ya Said Abdala na Salma Omar Zenny.

Akiwasilisha mada katika Mkutano huo Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Tamwa Mohd Khatib Mohd amesema Tamwa imetaka kuanzisha mpangilio maalum wa kufutilia mwenendo wa ushiriki wa wanawake katika hatuo zote za uchaguzi wa mwaka huu.

Sauti za Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Tamwa Mohd Khatib Mohd.

Nao Baadhi ya washiriki katika mkutano huo wa siku mbili ambao ni kutoka katika asasi za kiraia zinazoshughulika na wanawake, wanawake wa vyama vya siasa na Jumuiya za Wanawake wa Kiislamu wametoa maoni haya katika mkutano huo.

Sauti ya Washiriki.