Zenj FM

Jeshi la Polisi Kusini Unguja lasisitiza uwajibikaji wa wakaguzi wa shehia

23 May 2025, 3:23 pm

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP. Daniel Shillah

Na Omar Hassan.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP. Daniel Shillah amewahimiza wakaguzi wa Polisi waliopangiwa kufanya kazi katika Shehia mbalimbali kuwatumikia wananchi na kuwajengea mazingira tulivu ya kiusalama na kwamba atawachukulia hatua wakaguzi wasiofika katika Shehia walizopangiwa.
Akizungumza na Vikundi vya ulinzi shirikishi na wananchi wa Wilaya ya Kati huko katika Kijiji cha Uzi Mkoa wa Kusini Unguja Kamanda Shillah amesema suala la ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Wananchi katika kukabiliana na uhalifu ni muhimu na sio la kupuuzwa.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja.

Nae Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati, Mrakibu wa Polisi (OCD) Victor Ayo amesifu juhudi za Vijana wa vikundi vya ulinzi shirikishi kushirikiana na Jeshi la Polisi na kufanikisha kupunguza uhalifu katika wilaya hiyo.

Sauti ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati.

Kwa upande wake Mkaguzi wa Polisi Shehia ya Uzi Suleiman Zidi amewaomba wananchi wa Uzi na vijiji jirani kuzidisha ushirikiano na Wakaguzi wa Shehia zao kwani amesema wananchi wamekuwa wakifaidika na harakati zao za uzalishaji mali kutokana na ulinzi wa uhakika.

Sauti ya Mkaguzi wa Polisi Shehia ya Uzi Suleiman Zidi.