Zenj FM

Polisi Kusini Unguja kuimarisha ulinzi sikukuu ya Eid-el-fitr

29 March 2025, 6:21 pm

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Daniel Shillah.

Na Omar Hassan

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja litaimarisha ulinzi katika maeneo yote ya Mkoa huo kipindi cha Sikukuu ya Eid El Fitri ili wananchi washeherekee sikukuu hiyo kwa salama na Amani.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Tunguu, Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamanda wa Polisi Mkoa huo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Daniel Shillah amesema Jeshi la Polisi litahakikisha linabaini, kudhibiti na kutanzua matukio yote ya kihalifu.

Kamanda Shillah amewaonya madereva kutovunja sheria za usalama barabarani wanapochukua abiria kwenda katika viwanja na kumbi za starehe.

Aidha, amewataka wananchi katika Mkoa huo kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa Taarifa za viashiria vya uvunjifu wa Amani.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa huo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Daniel Shillah.