

24 March 2025, 5:49 pm
Naibu Mkurugenzi wa Upelelzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Naibu Kamishna wa Polisi Zuberi Chembera
akizungumza na Maafisa wa Polisi Wilaya na Wakuu wa Usalama Barabarani wa Mikoa ya Unguja
.Na Said
Naibu Mkurugenzi wa Upelelzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Naibu Kamishna wa Polisi Zuberi Chembera amewataka Askari Polisi kuwajibika na kuhakikisha wanasimamia sheria za usalama barabarani ili kupunguza vifo na majeruhi yanayosababishwa na ajali za barabarani.
Ameyasema hayo Makao Makuu ya Polisi alipokua akizungumza na Maafisa wa Polisi Wilaya na Wakuu wa Usalama Barabarani wa Mikoa ya Unguja amesema idadi ya ajali zilizosababisha vifo na majeruhi zimepanda asilimia 28.0 mwaka 2024 ukilinganisha na mwaka 2023.
DCI Chembera amesema ajali nyingi zinasababishwa na Uzembe wa Madereva wasiotaka kufata sheria, hivyo amewaagiza wakuu hao kuacha muhali na kuchukua hatua bila ya kumuonea
mtu.
Aidha amewataka wakuu hao wa barabarani kuendelea kushirikiana na Mamlaka ya leseni Zanzibar na kuwafutia leseni madereva wote wasio na sifa wanao sababisha ajali ili iwe fundisho kwa wengine.
Naibu Mkurugenzi wa Upelelzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Naibu Kamishna wa Polisi Zuberi Chembera
.