Zenj FM

Polisi Kusini Unguja kuimarisha ulinzi uandikishaji wa wapigakura

7 March 2025, 6:05 pm

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP. Daniel Shillah Akizungumza na waandishi wa habari huko Tunguu.

Na Omar Hassan

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP. Daniel Shillah amesema Jeshi la Polisi katika Mkoa huo limejipanga kuimarisha ulinzi katika zoezi la Uandishaji wa wapigakura ili kuweka mazingira ya utulivu kwa wanaojiandikisha na wananchi wengine.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Tunguu Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamanda Shillah amesema watahakikisha wananchi wanajiandikisha bila ya vurugu na bila ya vitisho na kwamba watakaojaribu kuvuruga zoezi la Uandikishaji watachukuliwa hatua kwamujibu wa sheria.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP. Daniel Shillah.

Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amewahimiza wananchi wenye sifa katika Mkoa huo kujitokeza kujiandikisha ili wapate fursa ya kuchagua Viongozi katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud.

Zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura linatarajiwa kuanzaa tarehe 8 marchi hadi 10 wilaya ya Kati na tarehe 11 hadi 13 kwa wilaya ya Kusini.