

6 March 2025, 7:14 pm
Na Omar Hassan.
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Kombo Khamis Kombo amewataka Askari wa Jeshi la Polisi kutumia maarifa wanayopata vyuoni kukabiliana na matukio ya uvunjifu wa Amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi Mkuu ili uchaguzi huo ufanyike kwa utulivu, salama na Amani.
Akifunga ya Mafunzo ya uongozi mdogo ngazi ya Sajenti kozi nambari 2, 2024/huko Chuo cha Polisi Zanzibar amewahimiza pia kutumia mafunzo hayo kukabiliana na uhalifu na wahalifu.
Akitoa tathmini ya Mafunzo Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar, Kamishna msaidia Mwandamizi wa Polisi
SACP. Moses Neckemiah Fundi amesema mafunzo hayo yaliyowahusisha Askari wanafunzi 1013 kutoka Mikoa yote ya Tanzania yametolewa kwa ustadi mkubwa, yatapelekea Askari hao kufanyakazi kwa kiwango kinachokubalika na kuwa viongozi bora.
Akisoma risala ya wanafunzi Koplo Peter Paul Mwakabenga wameahidi kuyafanyia kazi masomo waliyoyapata katika kulitumikia Taifa.