Zenj FM

Polisi watakiwa kutumia mafunzo kufanya mabadiliko ya kiutendaji

6 March 2025, 3:20 pm

Mkuu wa Operation na Mafunzo Polisi Kamisheni ya Zanzibar, Kamishna Masaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Matias Nyange akizungumza wakati Akifunga mafunzo ya Medani za kivita katika kambi ya Polisi Kiashange Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Na Omar Hassan,

Askari wa Jeshi la Polisi wametakiwa kutumia mafunzo wanayoyapata kufanya mabadiliko ya kiutendaji katika kutatua changamoto za kiusalama katika vituo vyao vya kazi. Akifunga mafunzo ya Medani za kivita katika kambi ya Polisi Kiashange Mkoa wa Kaskazini Unguja yaliyowahusisha Askari wanafunzi 1013 wa kozi namba 2. 2024/2025 Mafunzo ya uongozi Mdogo ngazi ya Sajenti, kwaniaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mkuu wa Operation na Mafunzo Polisi Kamisheni ya Zanzibar, Kamishna Masaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Matias Nyange amesema jamii inakabiliwa na changamoto za uhalifu wa kielektroniki, matumizi mabaya ya teknolojia na upotoshaji wa taarifa hivyo kuna umuhimu wa kutumia ujuzi, akili, busara na ushirikiano katika kufanikisha utatuzi wa changamoto hizo.

Sauti ya Mkuu wa Operation na Mafunzo Polisi Kamisheni ya Zanzibar, Kamishna Masaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Matias Nyange.

Nae Mkuu wa Mafunzo Chuo cha Polisi Zanzibar, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Pili Fobe amesema mafunzo waliyopewa Askari hao yatawafanya kuwa vingozi Mahiri katika himaya zao.

Sauti ya Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Pili Fobe.