Zenj FM

Polisi kuimarisha ulinzi zoezi la uandikishaji wa wapiga kura awamu ya pili

30 January 2025, 2:20 pm

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Kombo Khamis Kombo.

Na Omary Hassan.

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Kombo Khamis Kombo amesema Jeshi la Polisi limeweka mikakati ya kuimarisha ulinzi katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura awamu ya pili unaotarajiwa kuanza Febuari 1, 2025 ili zoezi hilo lifanyike kwa salama na Amani.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar CP. Kombo amewahimiza wananchi kuheshimu sheria na kujiepusha na vitendo vya uchochezi, lugha za matusi na vitendo vinavyoweza kuleta vurugu na kusababisha kuharibu Amani ya nchi.
Aidha ametoa rai kwa taasisi za Serikali, mashirika ya kiraia, taasisi za dini na vyombo vya habari kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhamasisha wananchi kuendelea kudumisha Amani na Utulivu.

Sauti ya Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Kombo Khamis Kombo.