

29 January 2025, 6:34 pm
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Kombo Khamis Kombo akikagua miradi ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya Vituo na nyumba kwa ajili ya maakazi ya Askari
Na Omar Hassan.
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Kombo Khamis Kombo amekagua miradi ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya Vituo na nyumba kwa ajili ya maakazi ya Askari ambapo amesema utakapokamilika ujenzi wa miradi hiyo itawafanya Askari kuishi na kutoa huduma katika mazingira Mazuri.
Akizungumza mara baada ya kukagua miradi hiyo huka katika Kikosi cha kutuliza Ghasia Mkoa wa Mjini Magharibi CP KOMBO amesema Miradi 15 inatekelezwa na Polisi Kamisheni ya Zanzibar kwa mwka wa fedha 2024/2025 ambayo itagharimu Zaidi ya shilingi bilioni 2.
Ametaja baadhi ya miradi mipya ambayo ameikagua na imeanza ujenzi ni pamoja na kituo kipya cha Polisi Bububu ambacho kitagharimu milioni 250, kituo cha Polisi Mwera milioni 350, ujenzi wa kituo cha Polisi Shauri moyo Sh. Milioni 115, kituo cha Polisi Dimani milioni 115, ujenzi wa Maktaba ya chuo cha Polisi Zanzibar milioni 100, ukarabati wa nyumba 3 za Polisi Tunguu milioni 291, ukarabati wa nyumba 10 kambi ya Polisi Ziwani milioni 376 na ukarabati wa Ofisi za Kikosi cha Kutuliza Ghasia miliomi 113.
Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama DKT. SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Polisi na kufanya kazi katika mazingira mazuri.