Zenj FM

Boti ya doria kupunguza uvuvi haramu Kusini Unguja

21 January 2025, 3:21 pm

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohd Mahmoud akizungumza wakati akikabidhi boti ya doria iliyotolewa na Shirika la Mwambao kwa kamati ya kamati ya uhifadhi wa mazao ya baharini iliyojumuisha vijiji saba vya Maeneo ya ukanda wa bahari ya ghuba ya chwaka.

Mary Julius.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohd Mahmoud amesema upatikanaji wa boti ya doria kwa kamati ya uhifadhi wa mazao ya baharini katika ghuba ya chwaka itasaidia kupunguza changamoto za mapambano dhidi ya vitendo vya uvuvi haramu.
Ayoub ameyaeleza hayo huko Kijiji Cha Marumbi wakati akikabidhi boti ya doria iliyotolewa na Shirika la Mwambao kwa kamati hiyo iliyojumuisha vijiji saba vya Maeneo ya ukanda wa bahari ya ghuba ya chwaka.
Amesema licha ya Serekali, wadau na kamati za uhifadhi kuendelea na juhudi za kupambana na vitendo hivyo lakini bado juhudi hizo zilikua hazifikii malengo kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo dhana duni hivyo kupatikana kwa boti hiyo kubwa na ya kisasa itasaidia kurahisisha shughuli za mapambano dhidi ya vitendo hivyo.
Aidha amesema Serekali haitasita kumchukulia hatua kali za kisheria kwa nvuvi yoyote atakaejihusisha na uvuvi haram huku akiwataka wanchi WA vijiji vya ghuba ya chwaka kulipa umuhimu suala la uhifadhi wa rasilimali za bahari ili ziweze kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohd Mahmoud.

Mkurugenzi wa Idara ya Uhifadhi wa Maeneo ya baharini Dkt Makeme Omar Makame amesema Serekali imekua ikitambua mchango mkubwa unaotolewa na wadau wa maendeleo na imewaekea mazingira Bora ya utekelezaji wa miradi na kwa sasa wanaendelea kutekeleza miradi mbali mbali ikiwemo ya uhifadhi katika sekta ya uvuvi na uchumi wa bluu kwa unguja na Pemba ili kwenda sambamba na azma ya serikali katika kuongeza uzalishaji wa mazao ya bahari.

Sauti ya Mkurugenzi wa Idara ya Uhifadhi wa Maeneo ya baharini Dkt Makeme Omar Makame.
Boti ya doria iliyotolewa na Shirika la Mwambao kwa kamati hiyo iliyojumuisha vijiji saba vya Maeneo ya ukanda wa bahari ya ghuba ya chwaka.

Mkurugenzi wa Shirika la Mwambao Zanzibar Said Khalid amesema shirika hilo litaendelea kuunga mkono juhudi za Serekali katika masuala ya uhifadhi wa bahari ili kuona rasilimali za bahari zinakua endelevu na ziaendelea kuwanufaisha wananchi hasa wa ukanda wa pwani na kujiongezea kipato.

Sauti ya Mkurugenzi wa Shirika la Mwambao Zanzibar Said Khalid.

Nae Mwenyekiti wa kamati ya uhifadhi ghuba ya Chwaka Masoud Mohd Abdalla amesama. Kupatiwa kwa boti hiyo itawasaidia kutekeleza Vyema shughuli zao za kupambana na vitendo vya uvuvi haramu na Wameahidi kuitunza na kuvitumia kwa lengo lililokusudiwa.

Sauti ya Mwenyekiti wa kamati ya uhifadhi ghuba ya Chwaka Masoud Mohd Abdalla.

Boti hiyo pamoja na vifaa vya uvuvi iliyogharim million 34 imetolewa na shirika la mwambao Zanzibar chini ya ufadhili wa shirika la world aids la Marekani kwa vijiji vilivyomo ndani ya ghuba ya chwaka ikiwemo Marumbi, Uroa, Michamvi, Chwaka, Charawe, Ukongoroni na Pongwe Pwani.