Mwakilishi Malindi Apongeza Serikali ya Awamu ya Nane kwa Miradi ya Maendeleo
24 December 2024, 4:16 pm
Na Mary Julius.
Mwakilishi wa Jimbo la Malindi Mohamed Ahmada Salum amesema serikali ya awamu ya nane chini ya Dk Hussein Ali Mwinyi imetekeleza kwa kishindo ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020- 2025 katika utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo,katika jimbo la Malindi.
Mwakilishi ameyasema hayo katika hafla ya kugawa vifaa na fedha kwa viongozi wa wadi za jimbo hilo hafla iliyofanyika katika wadi ya Gulioni, Amesema miradi hiyo ni pamoja ujenzi wa barabara za ndani, ujenzi wa skuli,ujenzi wa hospital pamoja na kuboresha huduma za maji, ambazo zimeleta manufaa kwa wananchi wa Malindi
Aidha mwakilishi Mohamed amepongeza jitihada za serikali katika kufanikisha maendeleo katika jimbo la Malindi, huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha mafanikio zaidi katika miaka ijayo.
Katika kuhakikisha jimbo la Malindi linaunga mkono juhudi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan katika matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia mwakilishi huyo amegawa majiko 200 ya nishati safi ya kupikia (gesi) kwa wajasiriamali waliopo katika jimbo hilo.
Kwa Upande Wao Madiwani Wa Wadi zilizopo Katika Jimbo Hilo wamempongeza mwakilishi kwa kuendelea kuunga kuunga mkono juhudi za rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi katika kuhakikisha jimbo hilo linakuwa la mfano wa kuigwa kwa maendeleo yake na wakazi wa jimbo hilo.
Kwa upande wake Katibu wa Wadi ya Mlandege amepongeza utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kwa jimbo la Malindi na kuwa ahidi kuwaunga mkono viongozi wa jimbo hilo.
Waliokabidhiwa vifaa hivyo ni pamoja na vilabu vya mpira wa miguu , kwa kupewa fedha taslimu, maskani kwa kupewa tv, wajasiriamali kwa kupewa nishati safi ya kupikia, mabalozi kwa kupewa fedha taslimu pamoja na ofisi za wadi kwa kupewa computer printa.